Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Babu Amlawiti Mjukuu Wake wa Kike.....Amhonga sh.2000 ili Asitoe Siri

Babu Amlawiti Mjukuu Wake wa Kike.....Amhonga sh.2000 ili Asitoe Siri

POLISI wilayani Masasi mkoani Mtwara inamshikilia mkazi wa kijiji cha Maili Sita kata ya Mtandi, Daudi Pilipili (44) kwa tuhuma za kumlawiti mjukuu wake wa kike mwenye umri wa 13.



Mkuu wa Polisi wilaya ya Masasi, Azaria Makubi alisema inadaiwa alitenda kosa hilo juzi saa 9:00 katika kijiji cha Maili Sita huku bibi wa mtoto akiwa amekwenda nyumbani kwa mwalimu wa shule anakosoma mjukuu wake (aliyelawitiwa) kwa mazungumzo.

Alisema siku ya tukio mzee huyo alimkamata mjukuu wake na kumwingiza chooni huku akimweka vitambaa mdomoni asitoe sauti na alipomaliza kitendo chake hicho cha kinyama alimpatia mtoto Sh 2,000 ili asitoe siri kwa wazazi wake.

Inadaiwa watoto wenzake ndio waliotoa taarifa hiyo baada ya kushuhudia kitendo hicho kikifanyika na polisi kutaarifiwa.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips