Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Tetesi za Kutimuliwa kwa Van Gaal zashika Kasi...

Tetesi za Kutimuliwa kwa Van Gaal zashika Kasi...

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Louis Van Gaal huenda akatupiwa virago na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho kabla ya mwisho wa mwezi Februari kwa mujibu wa gazeti la The Sun.

Kipigo cha 2-1 kutoka wa Sunderland Jumamosi kumewaacha mashetani wekundu na nafasi ndogo sana kumaliza nafasi ya nne msimu huu huku Ligi ya Uropa ndiyo michuano pekee wanayoweza kufuzu kwa ajili ya msimu ujao kucheza klabu bingwa barani Ulaya.

Mourinho amekuwa akitajwa sana kwenye tetesi za kibarua cha Man United licha ya nadharia zilizozuka kuwa huenda asiendane na tamaduni za klabu hiyo.

Inaaminika kuwa kwa hali hii hawawezi kutinga nne bora kabisa huku habari zinadai kuwa uongozi wa mashetani hao wekundu unaweza kusitisha mkataba wa Van Gaal na kumleta Mourinho sasa wakati wakilenga mechi dhidi ya Arsenal Februari 28 WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips