Nina rafiki yangu lakini tunaishi nchi tofauti tunakutana mara 3-5 kwa mwaka hua mie nikienda nchi anayoishi anakuja kunitembelea na yeye akija ninakoishi anafikia kwangu.Yeye hajabahatika kupata mtoto mwaka wa 5 sasa tangu ameolewa, jana wakati tuna kula akaniomba tuonge kitu muhimu baada ya chakula, nikamwambia inshallah tutaongea.
Basi baada ya chakula na mambo mengine nikaenda kuwalaza watoto nikaenda chumbani kwake haya nimekuja tuongee, basi akanambia kama unavyojua sina mtoto na nimejaribu dawa zote unazozijua za kizungu na miti shamba sijafanikiwa kupata ujauzito sasa tumeshauriyana na mume wangu nikamwambia changua rafiki yangu yoyote mimi nitaongea nae ili atupatie mtoto.
Mie macho niliyatoa nakutetemeka juu, nikamwambia sijafahamu unamaanisha nini ukisema rafiki yako akupe mtoto je unataka nikupe mwanangu ule au vipi? Kasema NO nataka ulale na mumewangu nilimshangaa lakini sikutaka ahisi vibaya ilibidi nijikaze nikamwambia na ilikuwaje nikawa mie?
Kasema ndani ya moyo wangu nili wish mume wangu akuchague wewe na aliposema bora wewe ndio nikafurahi zaidi.Waungwana nilimpa maneno mengi yakumpa moyo lakini naomba nisema kua sijakubaliana na ombi lake na nimemwambia anisamehe sitoweza kufanya hicho kitu ila nitamsaidia kwa hali na mali.
Nitamuulizia kwa watu kama kuna tiba lakini kwa mimi siwezi na mumewe pia niliongea nae nikamwambia wanisamehe sitoweza, je nimekosea kuwakatalia?
Sijapenda lakini sina choice naipenda Family yangu sana na hata hili jambo silifikishi kwa Mr.
By Nimpendenani/JF...WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment