Wema miss Tanzania 2006, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya safari yake ya kisiasa ambayo ameianzisha baada ya kushindwa kwenye uchaguzi ubunge viti maalum (CCM) mkoa wa Singida uliofanyika hivi karibuni.
Alisema matunda ya safari yake ya kisiasa yataanza kuonekana kuanzi oktoba mwaka huu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, kwani jimbo la Singida mashariki,litakuwa mikononi mwa CCM chama tawala.
“Mimi nimerudi Singida kwa kazi maalum, nimekuja kushiriki upigaji kura za maoni CCM.Tumemchagua mgombea wetu Jonathan Njau…..tutahakikisha Njau anamgaragara Tundu Lissu”,alisema Wema kwa kujiamini.
Akifafanua,alisema hivi sasa maandalizi ya kuing’oa CHADEMA jimbo la Singida mashariki,yameanza na yanaendelea vizuri.
Wema alisema kazi ya kuing’oa CHADEMA mwaka huu, itafanywa kwa ushirikiano wa karibu na wana CCM wote na kuungwa mkono na kundi la wasanii maarufu kutoka jijini Dar-es-salaam.
Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Aluu Segamba,amesema Wema ameonyesha amekomaa kisiasa kwa kitendo chake cha kurudi Singida mapema,licha ya kuangushwa kwenye uchaguzi wa ubunge viti maalum CCM hivi karibuni.
“Tunaendeleaa kushuhudia wana CCM wengi wanaoangushwa kwenye chaguzi mbalimbali,huwa na chuki na chama na wangine wamefikia uamuzi wa kukihama chama. Lakini Wema ndio kwanza mapenzi yake kwa chama yameimarika na sasa anaelekeza nguvu zake kulikomboa jimbo la Singida mashariki kutoka CHADEMA na kulirudisha CCM”, alisema Segamba. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment