Lionel Messi alipata kura 49 kati ya 56 zote zilizopigwa, huku Suarez akipata kura 3 na Ronaldo akiambulia kura mbili.
Pamoja na ushindi wa tuzo ya uchezaji bora wa bara la ulaya, Lionel Messi pia ametunukiwa tuzo ya goli bora la msimu uliopita katika michuano ya Champions League.
Goli la Messi liloshinda tuzo hiyo, ni goli ambalo alilifunga dhidi ya FC Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya msimu uliopita jijini Barcelona katika dimba la Nou Camp, Messi alifunga goli hilo kwa kumpiga chenga beki wa Bayern Jerome Boateng na kuinua mpira uliopita golikipa Manuel Neuer aliyehangaika kudaka bila mafanikio yoyote.
Rekodi za Lionel Messi msimu wa 2014/15
– 57 mechi alizocheza.
– 58 magoli aliyofunga
– 27 pasi za magoli alizotoa kwa wachezaji wenzie.
– 3 makombe aliyobeba.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment