Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar kulipokuwa na fainali za shindano la vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT 2015) ambapo Lulu alimpita mama huyo kama hawajuani kitendo ambacho kilisababisha minong’ono ukumbini hapo.
FrolaMtegoa“Inastaajabisha sana yaani huyu Lulu ndiyo kafikia hatua ya kumdharau mama Kanumba kiasi hiki, siyo siri hamtendei haki huyu mama sijui ni kitu gani kikubwa ambacho alimkosea,” alisikika mmoja wa mashabiki.
Mama Kanumba alipohojiwa na paparazi wetu ukumbini hapo, alisema anashindwa kumuelewa Lulu kwani hata ukiondoa undugu wake, bado kiumri ni mtoto anayepaswa kuheshimu wakubwa.
“Nimestaajabu sana kuona Lulu hanisalimii na isitoshe alijifanya kama hana habari na mimi utasema kuna kitu nimemkosea, wakati yeye ndiye anatakiwa ajishushe kutokana na yale yaliyotokea, ni dharau kubwa amenionyesha wakati aliwahi kuniomba msamaha huko nyuma kuhusu matukio yake hayahaya ya kuninunia,” alisema mama Kanumba.
Alipotafutwa Lulu, simu yake haikuwa hewani na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.
Source:Globalpublishers WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment