Baba mzazi wa mwanamuziki huyo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa ‘Baba D’. |
ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa baba Diamond, baada ya Tiffah kuzaliwa Agosti 6, mwaka huu, mama mzazi wa nyota huyo, Sanura Kassim a.k.a Sandra alimpigia simu mzazi mwenzake huyo na kumjuza kwamba wamepata mjukuu, jambo ambalo walilifurahia kwa pamoja.
Wakiwa katika mazungumzo hayo kwenye simu, baba Diamond alimuuliza kuhusu sura ya mtoto kama kweli ni wa kwao au siyo kama tetesi zinavyozagaa kwamba siyo wao ambapo alihakikishiwa na mama huyo kuwa Tiffah ni damu yao kwani anafanana na mtoto wao Diamond hasa mdomo.
BABA DIAMOND AFURAHIA
“Nilifurahi sana nilipopigiwa simu na mama Diamond na kuniambia tumepata mjukuu tulipongezana, pia nikamuuliza kuhusu wasiwasi wa kwamba siyo damu yetu kama wengi wanavyodai ambapo alinihakikishia kwamba ni damu yetu,” alisema baba Diamond.
AKATALIWA KUMUONA, APIGWA CHANGA
Baba Diamond alifunguka kuwa, wakiwa wanaendelea na mazungumzo, alimtaka mzazi mwenzake huyo amwelekeze nyumbani ili akamuone mjukuu wake, Tiffah lakini mama D alimpiga ‘changa la macho’ na kumwambia hawapo wameshasafiri kwenda nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
“Niliumizwa sana na maneno hayo kwani yalionesha wazi kwamba, mama D hataki niende kumuona, kwani nyombo vya habari kila siku vinaripoti kwamba Zari na mwanaye wapo hapa Bongo lakini nikaona isiwe shida nikapiga kimya tu,” alisema baba Diamond.
Hata hivyo, baba D alisema kuwa, kutokana na kupigwa changa hilo la macho, hakuweza kwenda kwani hajawahi kufika hata nyumbani kwa Diamond alikohamia huko Madale-Mivumoni jijini Dar na anaona sawa tu kwani hana la kufanya.
UKWELI NI HUU
Kwa mujibu wa mtu wa ndani kwenye familia ya Diamond, ukweli ni kwamba, Zari na mwanaye Tiffah mpaka sasa wako nyumbani kwao na hawajasafiri kwenda Sauz kama alivyoelezwa baba
Diamond mwenyewe hakuweza kupatikana kuzungumzia jambo hilo kwani muda wote simu yake ya mkononi haikupatikana hadi tunakwenda mitamboni.
Source:Globalpublishers WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment