Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » , , » Mbunge Edward Lowassa kakaribishwa UKAWA, amejiunga nao? Majibu ni haya kwa Mbatia… (Audio)

Mbunge Edward Lowassa kakaribishwa UKAWA, amejiunga nao? Majibu ni haya kwa Mbatia… (Audio)


“Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje” >>>> Hii ni moja ya sentensi ambazo Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliziongea Arusha May 30 2015 alipotangaza nia ya Kugombea Urais kupitia CCM.
LOWASSA
CCM ilikuwa na Wagombea zaidi ya 40 ambao walitangaza nia na kuchukua fomu za Kugombea Urais 2015 lakini baadae Chama hicho kikampitisha Dk. John Pombe Magufuli kugombea nafasi hiyo, baada ya hapo kukawa na headlines nyingi sana kuhusu ishu ya Edward Lowassa na UKAWA.
Viongozi wa Umoja wa UKAWA wamekutana Dar na mmoja wa Viongozi hao, James Mbatia amesema wamekubaliana kumkaribisha Mbunge Edward Lowassa ndani ya UKAWA na wako tayari kumpa nafasi na kushirikiana nae.
‘UKAWA tunahitaji viongozi wenye sifa, uwezo na weledi katika kulinda kuheshimu na kusimamia rasilimali za Taifa… Tunamwalika Edward Lowassa ajiunge na UKAWA na tuko tayari kushirikiana nae kuhakikisha tunaing’oa CCM madarakani kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.. Tunaamini ana uwezo wa kuhamasisha umma kuikataa CCM na udhalimu wake‘ >>>> James Mbatia.
Zimeandikwa stori nyingi kuhusu Mbunge huyo kujiunga CHADEMA, kingine kilichoibua maswali mengi ni ishu ya UKAWA kuchelewesha kumtaja Mgombea wao wa Urais… hapa ziko picha mbili zilizoenea Mitandaoni zikimwonesha Mbunge Edward Lowassa pamoja na Viongozi wa UKAWA, kuna chochote kinafuatia?
UKAWA
UKAWAII
Hapa iko sauti ya Mbunge James Mbatia akiongelea uamuzi huo.

WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips