Ngassa na Mkewe Radhia |
Mchezaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar, Azam FC na Simba SC, Ngassa ametua Johannesburg leo asubuhi na kuunganisha safari kwa gari la dogo la Free State kwenda Bethlehem.
Ngassa ametua na mkewe, Radhia Enea Mngazija na watakwenda kukagua nyumba aliyopewa na mwajiri wake, tayari kuanza maisha mapya.
Nimekuja huku kuhamia rasmi sasa, tunakwenda kuangalia nyumba mimi na bibie (Radhia). Unajua mambo ya nyumba ni ya akina mama. Sasa yeye akisema ameipenda nyumba, nawaambia safi, tunaingia,”amesema.
Hata hivyo, Ngassa atarejea Dar es Salaam wiki ijayo kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinachokwenda kucheza na Misri mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika katikati ya mwezi.
“Nadhani sitakuwa na muda mrefu, viongozi niliwaambia kabisa natakiwa kwenye kambi ya timu ya taifa. Kwa hivyo wanajua. Natarajia kurudi wiki ijayo tu kujiunga na timu ya taifa,”amesema.
Ngassa amejiunga na FS mwanzoni mwa mwezi huu kwa Mkataba wa miaka minne, kama mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake Yanga SC. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment