Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Uso Kwa Uso na Mke Wa Rafiki yangu Gesti

Uso Kwa Uso na Mke Wa Rafiki yangu Gesti

Wakuu weekend iliyopita nilimuaga mke wangu kuwa Nina semina nje ya dar kikazi maana hiyo ndo huwa mbinu yangu ya kwenda kwenye dhambi zangu kwa siku tatu NNE
Nilikua nime import mchepuko wangu kutoka arusha so nika check in kwenye hotel moja bagamoyo tukajipumzisha hapo alhamisi,Ijumaa, Jumamosi jumapili asubuhi tuka check out

Wakati nafunga mlango wa room nashtuka kumuona mke Wa Rafiki yangu akitoka Chumba mkabala na changu akiongozana na zee moja hivi nao wakifunga Chumba chao shemeji alitetemeka na kupata mshtuko mkubwa hadi yule Mzee kumuuliza kuna nini

Mchepuko wangu ulishatangulia kwenye gari nikamsalimia shemeji nikamwambia mm ndo na check out nilikua semina ya siku tatu ndo imeisha, akaitikia kwa kichwa tu,
Nikapiga hatua za haraka kwenda kwenye Gari ili asiuone mchepuko wangu ambao ulishatangulia kwenye gari

Jumatatu akanipigia simu mwenyewe akaniambia shemeji naomba unifichie siri sitarudia tena
Nikamwambia naomba tuongee baadae kwa sasa nipo busy

Mchana wake akanitumia meseji inasomeka hivi "" Shem naomba kama vipi tafuta sehemu nije tumalizane kiutu uzima and you stay silence forever "" naomba unijibu i can't afford to loose this marriage

Wakuu nipo njia panda, ingawa mm ni mzinzi na sina utakatifu lakini siwezi kutembea na mke Wa Rafiki yangu kipenzi tulieshibana miaka nenda miaka Rudi
Na nilishawahi kukaa kwake sana wakati sijapata kazi yy alianza kuja dar kabla yangu

Kwa sasa huyu jamaa yupo mkoani kikazi alihamishiwa huko mke alishindwa kumfuata kwa yy mwenyewe ana kazi hapa dar .

Jana kanitumia M-PESA laki tano ikisindikizwa na msg kuwa vipi shemeji lile suala letu umeamuaje ukimya wako unaniumiza.
Sikujibu kitu

Wakuu naomba muongozo wenu
Kweli nisimwambie Rafiki yangu kuhusu uzinzi Wa mkewe?

Na mm ndo nimepewa jukumu la kumuangalizia familia yake kwa mambo mbali mbali kwa kuwa yupo mbali

Nawasikiliza wakuu

By Montana WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips