Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Zitto awajibu CHADEMA juu ya fedha za ziara za ACT- Wazalendo mikoani

Zitto awajibu CHADEMA juu ya fedha za ziara za ACT- Wazalendo mikoani

Kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwa anashangazwa na viongozi wa CHADEMA kuhoji anakotoa fedha za kugharamia mikutano na ziara za ACT-Wazalendo pamoja na kujinadi kwa wananchi.

Zitto amewajibu jibu jepesi kwa kusema “CHADEMA walianza bila ruzuku, waulizeni fedha za ziara zao za kuzunguka kwa helkopta nchi nzima walizitoa wapi? Kule walikopita ndiko na mimi ninakopita huku na huko” alisema huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha

Alifafanua kuwa fedha za chama chake wanazofanyia ziara zinatokana na michango mbalimbali ya watu wenye nia njema na chama hicho, Zitto pia aliwataka wananchi wa Mwanza kuchuja na kuchagua uzalendo. “Chujeni mtu mwenye hoja twendeni tukaijenge nchi” WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips