Zimebaki siku 9 kabla ya pambano lilopewa jina la ‘Fight of the Century‘ kati ya mwanasumbwi tajiri zaidi duniani Floyd Mayweathe Jr ambaye
ana rekodi ya kutopoteza pambano hata moja tangu aanze kucheza mchezo
huo, dhidi ya mfilipino mwenye rekodi nzuri kabisa Manny Pacquiao kufanyika, leo hii bei ya viingilio vya kutazama mchezo huo imetangazwa.
Unaambiwa
tiketi ya bei ya chini kabisa itakayokuwezesha kuingia MGM Grand Garden
Arena itakuwa ikiuzwa kwa dola 1500 ambayo ni zaidi ya millioni 2.5 kwa
hela yetu TZ.
Kwa wale vibopa ambao wa kati tiketi zao zitauzwa kwa dola 7500.
Tiketi hizi zitaanza kuuzwa leo usiku saa 2 kwa saa za Marekani ambapo jumla ya ticket zitakazouzwa ni ticket 1000.
Wakati huo
huo zimetengwa tiketi za bei ya juu zaidi ambazo zitakuwa kwa ni dola
10,000 huku nyingine zikiuzwa kwa dola 200,000 kwa watu mashuhuri wenye
uwezo wao yani.
Pia kwa wale
watakaoshindwa kulipa viingilio hivyo, umeandaliwa mpango kuandaa sehemu
itakayoingiza watu 50,000 ambao watalipa viingilio dola 150.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment