Mfano wa Bastola iliyokutwa |
MAPYA
yamezidi kuibuka katika sakata la Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Joseph Gwajima, baada ya kuthibitika kwamba bastola iliyokamatwa katika
harakati za kile kinachotajwa kutaka kumtorosha kutoka katika Hospitali
ya TMJ, Dar es Salaam, ni mali yake.
Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema jana kuwa
uchunguzi wa kina na wa kitaalam, sasa umethibitisha silaha hiyo
inamilikiwa kihalali na Askofu Gwajima.
“Kuhusu
risasi 17 za short gun ni kwamba Askofu Gwajima anamiliki bunduki aina
ya short gun yenye namba 102837 ambayo inatumia risasi za aina ya hizo
zilizokamatwa,” alisema Kamanda Kova.
Bastola hiyo
ni moja ya vitu walivyokamatwa navyo wafuasi 15 wa Gwajima, wanaodaiwa
kula njama za kutaka kumtorosha usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
My Take: Najiuliza tu kwa sauti je ? Wachungaji kumiliki silaha inaingia akilini? Nilitegemea wanategemea sana ulinzi wa Mungu
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment