Nay amesema watu hao pia wanadai kuwa bangi ndizo zinampotezana kufanya muziki ambao waliamini kuwa unaleta chuki au usingeweza kumtoa na kumtabulisha kama wasanii wengine ambao walitamba kipindi hicho yeye akitafuta kutoka.
Nay wa Mitego alisema kuwa katika kuhangaika na muziki ilifika mahali hata mzazi wake ambaye ni mama yake mzazi alimfukuza nyumbani kwake akiwa darasa la saba sababu ya muziki ambao leo umeweza kumfungulia njia na kumpa mafanikio ambayo hata mzazi huenda anayafurahia.
"Wakati Naanza kila mtu aliniona kama napoteza muda hivi, wengine walisema bangi ndo zinanipoteza. Ata mama mzazi alinifukuza nyumbani nikiwa darasa la Saba sababu ya huu Muziki ninao ufanya sasa."
Mbali na kukatishwa tamaa Ney anadai kuwa hakuweza kukata tamaa sababu alikuwa anatambua nini anakifanya hivyo alizidi kukomaa na kuona kuwa anafikia malengo yake ya kufanikiwa kupitia muziki wa Bongo Fleva na kupata heshima hata kwa watu ambao walikuwa wanaona anapoteza muda.
"Sijawahi kukata tamaa nikiamini siku moja nitakuja kufanikiwa na wataniheshimu wote wanaonidharau..Thnx God kwa kunipa moyo wa ujasiri mpaka nilipo Leo..!! Angalau naheshimika, nackilizwa..Wengi wao leo wanajivunia Ney-Wamitego"
Mkali huyo kupitia ukurasa wake wa Instragram amewataka vijana kutokata tamaa na wazidi kutafuta pesa kwani hata yeye moja ya ndoto yake ni kuona anaishi maisha ya kitajiri na anaamini yatatimia hivi karibuni.
"Washkaji zangu eeh!?? Tutafuteni #Hela tuacheni masihara kabisaa.Kiukweli mimi napenda kuishi maisha mazuri yakitajiri (like a boss) na nina imani nitaishi ivyo soon, coz nikikumbuka nilikotoka daah..!!! Huwa sometimes siamini kama ni Mimi (Ahsante Muziki_Media_Mashabiki).WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment