Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akifafanua jambo kuhusiana na mshindi wa shilingi Milioni 100/-kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo Mkazi wa kilolo mkoani Iringa Bi.Uwezo Magedenge aliibuka na ushindi wa kitita hicho katika droo ya 14 iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam leo,Wengine ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Millao(Kushoto) na Afisa wa kampuni hiyo Pristin Lyatonga.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544
Magedenge binti mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni mhudumu wa mapokezi katika nyumba ya wageni ya Luganga Lodge iliyopo wilayani Kilolo amesema kuwa amepokea taarifa hizi kwa furaha akiwa kazini na amefurahia ushindi huu ambao anaamini utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.
“Katika maisha yangu nimeishapitia mambo mengi nahangaika na maisha hadi kufikia hapa nilipo nikiwa mhudumu kwenye nyumba ya wageni.Kwa ushindi huu naamini nitafungua shughuli zangu za biashara ikiwemo kuanzisha biashara ya maduka ya M-Pesa pia kufungua nyumba yangu ya kulala wageni na kusaidia ndugu zangu ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha,” alisema.
“Nashukuru Vodacom kwa kuleta promosheni hii ambayo naamini itabadilisha maisha yangu na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniona na kusikiliza sala zangu.”
Aliongeza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akishiriki kwenye promosheni mbalimbali na hajawahi kufanikiwa kwa ushindi huu anaamini kuwa promosheni hizi hususani za Vodacom ni za kweli na amewataka wateja wote kushiriki ili kutopoteza bahati zao za kujishindia mamilioni ya fedha na kubadilisha maisha yao.
Akiongea muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi, Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Rene Meza amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-
Naye Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja 2 wamekwishajishindia milioni 10 na wateja watano wameishajishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.
“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya kumi na nne hivyo bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.”
~Bongo5WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment