Mtangazaji na muigizaji wa filamu, Bond Bin Salim ‘Bond’ hivi karibuni amemtupia kijembe msanii na Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Five Efects,’ William Mtitu kwa kumwambia kuwa msemo wake wa kuwazika watu yeye ndiye anawaua?
“Namshangaa Mtitu, naomba ahojiwe, je, yeye ndiye anawaua wasanii? Kwa nini anapenda kusema mimi ndiyo nitakuzika siyo Mhindi?” alihoji Bond.
Baada ya kijembe hicho mwandishi wetu alimwendea hewani Mtitu ambaye alifafanua msemo wake na kusema: “Mimi ninavyojua huo ni msemo, hivi wasanii wakifariki si tunazikana wenyewe kwa wenyewe? Je, kuna ubaya gani wa kusema mimi ndiyo nitakuzika? Sipendi kumuongelea Bond kwa sababu ni mdogo sana kwangu na mimi siwezi kugombana naye, natumia busara za ukubwa wangu,” alisema Mtitu.
GPL
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment