Kupitia kipindi cha Clouds 360 mkuu wa wilaya ya kinondoni Paul Makonda katika mahojiano maalumu kuhusu issue ya Walimu wa shule za serikali Jijini Dar es salaam kupanda daladala bure, amesema jambo hilo sio lazima na hivyo kwa mwalimu atakaye liona halina tija basi aendelee kutumia nauli yake kama kawaida.
Hatua hiyo imefuata baada ya kuzuka minon’gono kuwa kuna baadhi ya walimu wanadai mpango huo huenda ukawadhalilisha kama wanavyo dhalilishwa wanafunzi katika vyombo hivyo vya usafiri hasa watakapo ombwa waoneshe vitambulisho vyao.
Hata hivyo Makonda amesema walimu na jamii kwa ujumla inapaswa kutambua kuwa kila mwanzo wa jambo kuna changamoto mbali mbali, lakini katika hili ameweka wazi mpango wa kuandaa vitambulisho maalumu kwa ajili ya walimu ili kuhakikisha wanatambulika kwa nafasi yao,
Makonda amesema anaimani asilimia kubwa ya watoa huduma ya daladala wengi wao walifundishwa na walimu hao kwa hivyo sio rahisi mtu kumdhalilisha mwalimu wake.
Baada ya mazungumzo kati ya wamiliki wa daladala na mkuu huyo wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam kukamilika huduma hiyo kwa walimu itaanza Siku ya Ijumatatu Machi 7, 2016.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment