Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Baba aua Binti yake, Amzika Nyumbani Kwake

Baba aua Binti yake, Amzika Nyumbani Kwake

JESHI la Polisi Mkoa wa Kagera, linamshikilia Gerald Paulo (34) kwa kosa la kumpiga binti yake, Anisia Gerald (14), sehemu mbalimbali za mwili wake na kumyonga kwa kutumia kanga.

Akizungumzia tukio hilo mjini hapa juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera,  Henry Mwaibambe, alisema tukio hilo lilitokea Mei 7, mwaka huu katika Kijiji cha Rugazi Kyaitoke kisha alichimba kaburi nyuma ya nyumba yake na kumzika.

Alisema walipata taarifa kutoka kwa jirani ya Paulo kuwa ameua binti yake na walipofuatilia walibaini ni kweli.

Alisema baada ya polisi kufukua kaburi hilo walikuta mwili wa binti huyo ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na kipande cha kanga shingoni.

Kwa taarifa nilizonazo, Gerald si mara ya kwanza kufanya mauaji kama hayo, maana miaka mitano iliyopita aliwahi kuua mtu na kukimbilia Karagwe kwa jinsi hiyo hiyo, kwa tukio hili lazima sheria zichukue mkondo wake,” alisema Mwaibambe. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips