Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Picha: Range Rover ya AY yamdatisha Daz Baba, asema AY ni mfano wa kuigwa

Picha: Range Rover ya AY yamdatisha Daz Baba, asema AY ni mfano wa kuigwa

Msanii wa zamani wa kundi la Daz Nundaz, Daz Baba amemmwagia sifa kibao rapper Ambwene Yessayah aka AY kuwa ni msanii wa kuigwa.
AY alitinga kwenye mazishi ya Mzee Ebby Sykes akiwa kwenye Range Rover ya rangi ya kijivu kitu ambacho kilimvutia Daz Baba...


Daz ameiambia Bongo5 kuwa AY ni mshikaji wake toka kipindi cha nyuma na anavutiwa na hustle zake.


AY akiondoka katika makaburi ya Kisutu baada ya mazishi ya Ebby Sykes akiwa kwenye Range Rover

“AY yuko vizuri sana, ni mfano wa kuigwa, mzee wa commercial toka kitambo anafanya muziki mzuri ndo maana unamuona hivyo, ” alisema Daz. “Jamaa anajituma, anafanya kazi kwa bidii ndio maana unaona hayo mafanikio yote,” aliongeza.

Pia Daz amesema kuna mpango wa kufanya ngoma na muimbaji huyo wa ‘Zigo’.

“Nina mpango wa kufanya naye kazi. AY ni mshkaji wangu toka kitambo kwahiyo kila kitu kitaenda sawa.”WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips