Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Lazaro Nyalandu na Aunt Ezekiel Wachanwa Bungeni Kuhusu Safari ya Kwenda Kutangaza Utalii

Lazaro Nyalandu na Aunt Ezekiel Wachanwa Bungeni Kuhusu Safari ya Kwenda Kutangaza Utalii


Jana wakati mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema , akichangia  hoja Bungeni nakudai kuwa mawaziri wengi  hawana ubunifu nakumrushia “bomu”  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuwa anazunguka nje ya nchi na msichana kwa madai ya kutangaza utalii.

Lema alisema;



“Angalia Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alikwenda kutangaza utalii nje ya nchi akiwa ameongozana na (mwigizaji maarufu wa filamu wa Tanzania) Anti Ezekiel,” alisema na kuongeza kuwa waziri huyo hashindi ofisini kwa kisingizio cha kutangaza utalii.

Picha za wawili hawa wakiwa nchini Marekani  wakitangaza utalii zilisambaa sana mtandaoni mwaka jana na kizua stori nyingi juu kile kilichofanyika.

Picha : Waziri Nyalandu akiwana Aunty Ezekiel pamoja na DJ Luke (wakatikati) wakitangaza Utalii, New York, Marekani.

Lakini hivi kuna ubaya gani Staa wetu kushirikiana na waziri katika kutangaza UTALIIII?!!!!WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips