Waku habari za mchana,kama nilivyojieleza hapo juu,ni kwamba
nilibahatika kuoa miaka 10 iliyopita iliyopita,tulipata sakrament ya
ndoa takatifu tar.7/5/2011.pia katika ndoa yetu tumejaliwa kupata watoto
2.sasa kilichonifanya nije hapa jukwaani ni taarifa nilizozipata toka
kwa jirani yangu ambae amenithibitishia kuwa mke wangu anatembea na mtu
ambae pia ni jirani yetu kabisa.mke wangu huwa anashinda nyumbani
akijishughulisha biashara ya kiduka tulichokifungua karibia mwaka
sasa.pia mimi huwa nashinda kibaruani kwangu ambapo mara nyingi huwa
nachelewa kurudi nyumbani kutokana na kabiashara kangu kanakonipatia
riziki.huyu jirangu kanijulisha huwa wanatoka majira ya saa 1 jioni na
kurudi sa 2:30 jioni kabla mimi sijarudi.baada ya kupata tarifa hizi
nilijaribu kufanya uchunguzi na nimeanza kuona kuna ukweli juu ya jambo
hili.juzi ilipofika saa 1:30 jioni nilimpigia simu kumuulizia jambo
fulani nikasikia anaongea taratibu tofauti na siku nyingine,nikamuuliza
umeshafunga duka?akanijibu ndio,nikamuuliza mbona mapema akasema kuna
mkanda nimeupenda nauangalia..nikakata simu nikampigia yule jirani
kumuuliza kama mke wangu yupo nyumbani akasema hayupo na ametoka na
jamaa kama kawaida yake,kama huamini uje uone.nilitamani kwenda lakini
nilishindwa kujua ni uamuzi gani nichukue kwa sababu,kwanza sikujua
wamekwenda guest gani,huyo jamaa anausafiri hivyo wanauwezekano wa
kwenda nje ya mji kidogo.nilijikaza sikumuuliza wala kumwonyesha dalili
zozote za kufahamu mambo hayo machafu anayoyafanya mke wangu.hivyo
naombeni ushauri wenu pindi nikiwafumania au kuwahi kurudi home na
kumkosa mke wangu wakati amenijulisha yupo home..naombeni ushauri wenu
ni uamuzi gani naweza kuchukua ukawa sahihi.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Home »
» Nasubiri Kumfumania Mke Wangu, Naombeni Ushauri
Nasubiri Kumfumania Mke Wangu, Naombeni Ushauri
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja
Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog
0 comments:
Post a Comment